Thursday, July 16, 2020

Membe: Nilifukuzwa kwa aibu kisa nimeonyesha nia ya kugombea urais

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje,Bernard Membe amesema alifukuzwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa sababu alitaka kugombea urais katika uchaguzi Mkuu ambao unatarajia kufanyika Oktoba.

Membe ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumza na wanachama wa ACT-Wazalendo baada ya kujiunga na chama hicho.

Amesema amefukuzwa kwa aibu na kutukanwa na vijana ambao unaweza kuwazaa licha ya kwamba hakutenda kosa lolote.

“Sikutenda kosa lolote. Kosa nililolifanya ni kuonyesha nia ya kutaka kugombea urais mwaka 2020 wanaosema nitaenda na kurudi, nitarudi wapi milango imefungwa,”  amesema Membe



source http://www.bongoleo.com/2020/07/16/membe-nilifukuzwa-kwa-aibu-kisa-nimeonyesha-nia-ya-kugombea-urais/

No comments:

Post a Comment