Thursday, July 16, 2020

Membe awapiga kijembe walioondoka CCM na kurudi ‘Mimi sio kama yule aliyeondoka na kurudi’

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe, amesema ameingia kwenye chama cha ACT-Wazalendo kwa sababu ni chama makini ambacho kinataka mabadiliko.

Membe amesema maamuzi aliyoyafanya sio kama yale ya mwenzake  aliyetoka na kurudi.

“Nimefukuzwa kwa aibu nimetukanwa na vijana ambao ninaweza kuwazaa na sikutenda kosa lolote. Kosa nililolifanya ni kuonyesha nia ya kutaka kugombea urais mwaka 2015 na 2020 wanaosema nitaenda na kurudi, nitarudi wapi milango imefungwa,”  amesema Membe

“Nimebaki mlangoni lakini chumba sijafika ila chumba ni kizuru hicho. Nineingia ACT-wazalendo,” amesema.

Amesema milango ya ikulu ipo wazi kulikoni miaka mingine tangu nchi ilivyopata Uhuru.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/16/membe-awapiga-kijembe-walioondoka-ccm-na-kurudi-mimi-sio-kama-yule-aliyeondoka-na-kurudi/

No comments:

Post a Comment