Monday, July 20, 2020

Zaidi ya Wafungwa 20 Waambukizwa Covid-19

coronavirus-covid

Maafisa wa polisi katika vituo hivyo wamepimwa corona, wanasubiri matokeo. Picha: Hisani

Kati ya wafungwa hao, 3 walikuwa Thika na 17 Makongeni

Maafisa wa polisi katika vituo hivyo wamepimwa corona, wanasubiri matokeo

Maafisa wa polisi sita wamepatikana na virusi vya corona tangu Machi 2020, Kiambu

Zaidi ya washukiwa 20 wamepatikana na virusi vya corona katika vituo vya polisi vya Thika na Makongeni kaunti ya Kiambu, Kenya.

Kulinagana na kamanda wa polisi katika kaunti hiyo Bw. Ali Nuno, visa  vitatu vilipatikana katika rumande ya Thika huku wengine 17 wakiwa katika kituo cha polisi cha Makongeni.

Kodiaga Prison International Bridges to Justice

Washukiwa kwenye rumande. Picha: Hisani

‘’ Vipimo hivyo vilifanyika wiki jana baada ya wawili kuonyesha dalili za covid,’’ alisema.

Wagonjwa hao sasa wametiwa karantini huku wakipata matibabu kuhusiana na virusi hivyo.

Aidha, alisema kuwa maafisa wa polisi katika vitu hivyo walipimwa na walikuwa wakisubiri matokeo baada  ya kutangamana na wagonjwa hao.

Nuno aliongezea kuwa maafisa wake sita katika kaunti hiyo wamepatikana na virusi vya corona tangu Machi 2020.

Virusi vya corona vimezidi kuwa tishio huku idadi ya maambukizi ikizidi kuinuka kila siku.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/20/zaidi-ya-wafungwa-20-waambukizwa-covid-19/

No comments:

Post a Comment