Monday, July 20, 2020

Rais Magufuli amesema wamejitokeza wagombea 10,367 kutaka ubunge, ataka kura zihesabiwe hadharani

Rais John Magufuli amesema jumla ya watu 10,367 wamejitokeza kuwania ubunge katika Chama cha Mapinduzi (CCM) jambo ambalo halijawahi kutokea.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati akiwaapisha aliowateua hivi karibuni.

Amesema fomu zilizochukuliwa ni 10,367 na waliorejesha ni 10,321 ziekamilika na ambao hawakurejesha 46.

“Haijawahi kutokea katika chama kimoja  katika ubunge wamejitokeza katika nafasi hiyo,” amesema Rais Magufuli.

Aliongezea kuwa “Kura za maoni zitanaza leo na kesho na matumaini watasimia kwa haki bila kuwepo na mizengwe,”.

Aidha, amesema watakaosimamia uchaguzi huu kwa leo na kesho hizo kura zihesabiwe kama Halmashuri Kuu walivyofanya hadharani ili kuwepo na uwazi.

“Uwazi huu utasaidia kujenga umoja wa CCM. kura zihesabiwe hadharani mbele ya wajumbe huko ndio kukua kwa demokrasia,”



source http://www.bongoleo.com/2020/07/20/rais-magufuli-amesema-wamejitokeza-wagombea-10367-kutaka-ubunge-ataka-kura-zihesabiwe-hadharani/

No comments:

Post a Comment