Monday, July 20, 2020

Gwajima Afunguka Ubunge Kawe “Nataka Kupanua Huduma”

Askofu Gwajima Achukua Fomu ya Kugombea Ubunge Jimbo la Kawe ...Askofu wa kanisa la Ufufuo na uzima Josephat Gwajima amesema kuwa hawezi kuacha kazi ya kanisa kwa sababu ya kugombea ubunge kama watu wengi wanadhani baada ya kutangaza nia ya kugombea kwenye jimbo la Kawe.

Akizungumza kanisani Kwake Ubungo Gwajima amesema anachokifanya ni kupanua huduma na si kwamba anacha kazi aliyotumwa na Mungu.

“Gwajima aachi huduma na kwenda kwenye siasa Gwajima aachi huduma kwenda kugombea ubunge anachikifanya Gwajima ni kupanua huduma nilikuwa nahudumia watu wa Ubungo tu ninachokitaka ni kusaidia nchi nzima, kutunga sheria za kuwasaidia watu wasiwe na mizigo mikubwa nataka niwape wananchi nchi nzima maji na chakula” amesema.

Mapema Julai 14,2020 kiongozi huyo wa kanisa alifika kwenye ofisi za chama cha mapinduzi (CCM) kuchukua fomu kwa ajili ya kuomba kuchaguliwa kupeperusha bendera ya chama hicho kwenye nafasi ya ubunge jimboni Kawe.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/20/gwajima-afunguka-ubunge-kawe-nataka-kupanua-huduma/

No comments:

Post a Comment