Wednesday, July 15, 2020

WHO Yatoa Onyo Kali Kuhusu Maambukizi Zaidi ya Covid19

COVID-19 pandemic will get worse if basic precautions aren't followed - WHO boss warns

Tedros ameeleza kuwa janga la corona litakuwa na madhara zaidi  iwapo tahadhari ifaayo haitachukuliwa. Picha: Hisani

Mkurugenzi mkuu wa shirika la WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus ameeleza kuwa nchi kadhaa zinaelekea pabaya

Tedros ameeleza kuwa janga la corona litakuwa na madhara zaidi  iwapo tahadhari ifaayo haitachukuliwa

Kiongozi wa idara ya mambo ya dharura katika shirika hilo alizishauri nchi kutofungua shule hadi makali ya virusi hivyo vipungue

Shirika la afya ulimwenguni WHO imeyatahadhisha mataifa kuhusu kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya corona iwapo hayatachukua kanuni za kukinga maambukizi hayo kwa uzito.

Mkurugenzi wa shirika hilo Tedros Adhanom Ghebreyesus ameeleza kuwa mataifa mengi yanaelekea pabaya haswa kutokana na kutozingatia kanuni zilizotolewa na shirika hilo.

Akizungumza katika mkutano wa kimtandao Jumatatu, Julai 14,  Tedros alieleza kuwa  kati ya visa vya maambukizi 230,000 vilivyoripotiwa Jumapili, Julai 12, 10% vilitoka katika nchi 1 huku 80% vikiwa vya nchi mbili pekee.

‘’Iwapo kanuni hazitafuatwa, janga hili litaongezeka- itakuwa mbaya zaidi na hatari zaidi,’’ Tedro alisema.

Kiongozi huyo alieleza kuwa janga la virusi vya corona lingali adui kubwa kwa ulimwengu.

Kauli yake inajiri wakati janga hilo limeambukiza zaidi ya watu takriban 13, 249,575 na zaidi ya vifo nusu milioni.

Kwingineko, Kiongozi wa idara ya mambo ya dharura Mike Ryan alitoa onyo kwa mataifa kuhusu kutofungua shule hadi makali ya virusi vya corona vinapopunguka.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/15/who-yatoa-onyo-kali-kuhusu-maambukizi-zaidi-ya-covid19/

No comments:

Post a Comment