Tuesday, July 14, 2020

Waziri Angela Kairuki, Dk Mpango na Bashungwa wamechukua fomu leo za kugombea

Waziri wa Uwekezaji, Angellah Kairuki amechukua fomu ya kugombea Ubunge jimbo la Same Magharibi kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).

Waziri huyo amekabidhiwa fomu huyo leo na Katibu wa CCM Wilaya ya Same, Victoria Mahembe.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa kuwania ubunge wa jimbo la Buhigwe.

Naye Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa, amechukua fomu katika Wilaya ya Karagwe kutetea uwakilishi wa jimbo la Karagwe.

 

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/14/waziri-angela-kairuki-dk-mpango-na-bashungwa-wamechukua-fomu-leo-za-kugombea/

No comments:

Post a Comment