Tuesday, July 14, 2020

Mrisho Gambo ajitokeza kuchukua fomu ya Ubunge ataka kumng’oa Lema

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Arusha, Mrisho Gambk amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea ubungr jimbo la Arusha Mjini kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Mrisho alitinga katika ofisi hiyo akiwa ameongozana na watoto wawili.

Jimbo hilo lilikuwa linashikiliwa na aliyekuwa mbunge wa Chadema, Godbless Lema.

Hivi karibuni Rais John Magufuli alimtumbua Mrisho katika nafasi ya Mkuu wa mkoa pamoja na Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi kwa madai ya kwamba wamekuwa wakigombana mara kwa na kukwamisha maendeleo.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/14/mrisho-gambo-ajitokeza-kuchukua-fomu-ya-ubunge-ataka-kumngoa-lema/

No comments:

Post a Comment