Tuesday, July 14, 2020

Madagascar: Wabunge 2 Wafariki Kutokana na Covid19 Licha ya Kuzinduliwa Tiba

Madagascar: COVID-19 kills 2 MPs as hope in country's much-hyped herbal remedy fades

Tanzania ilikimbia nchini humo kununua dawa hiyo kuwatibu wananchi wake. Picha; Hisani

Rais wa Madagascar  Andry Rajoelina alitangaza Jumapili kuwa wabunge wake wawili walifariki baada ya kuambukizwa virusi vya corona

Maseneta wengine 14 pamoja na manaibu wao 11 pia waliambukizwa virusi hivyo

Nchi hiyo ililazimika kuifunga tena mji mkuu wa Antananarivo kwa mara ya pili baada ya maambukizi ya virusi hivyo kupanda maradufu

Maseneta wawili wa Madagascar wamefariki kufuatia maambukizi ya virusi vya corona licha ya nchi hiyo kuzindua kile walichokitaja kama tiba kwa virusi hivyo.

Madagascar: COVID-19 kills 2 MPs as hope in country's much-hyped herbal remedy fades

Rais Andry Rajoelina alizindua tibaya corona. Picha: Hisani

Rais wa nchi hiyo Andry Rajoelina alieleza kuwa mwanachama mmoja wa seneti pamoja na naibu alifariki kutokana na ugonjwa huo huku wangine 25 wakipatikana na virusi hivyo.

Nchi hiyo ilichukua hatua ya kutangaza marufuku wa kuondoka nje katika mji mkuu wa Antananarivo baada ya maambukizi ya virusi hivyo kuongezeka miezi miwili baada ya kuondolewa marufuku hiyo.

Sokomoko ilizuka kati ya waandamanji na polisi nchini humo, wananchi wakiandamana kukashifu hatua iliyochukuliwa na serikali kufunga baadhi ya maeneo ya  taifa hilo.

Vurugu hivyo vilizuka baada ya mwanabiashara mmoja kudaiwa kupigwa na maafisa wa polisi kwa kukiuka kanuni za biashara kuhusiana na covid19.

Hadi sasa, hakuna aliyejitokeza kuzungumza lolote kuhusu dawa ya kienyeji iliyozinduliwa nchini humo  na Rais Andry, ikidaiwa kutibu virusi vya corona licha ya vifo kuripotiwa.

Rais Andry aliipa dawa hiyo umaarufu nchi Tanzania ikiwa mojawapo ya nchi kukimbia nchini humo kununua dawa hiyo kuwatibu wananchi wake.

Hadi sasa Julai 14, Madagascar imerekodi takriban maambukizi 5,080 vya virusi vya corona, waliopona 2,494 pamoja na vifo 37.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/14/madagascar-wabunge-2-wafariki-kutokana-na-covid19-licha-ya-kuzinduliwa-tiba/

No comments:

Post a Comment