Friday, July 17, 2020

Watu wawili wamefariki katika ajali ya basi na kujeruhi 28

Watu wawili wamefariki katika ajali ya Basi la Kyela Express na kujeruhi 28 ambao kati yao watatu wapo katika hali mbaya.

Basi hilo lililokuwa likitoka Dar es Salaam kwenda Wilayani Kyela limepinduka usiku wa kuamkia leo katika njia panda ya Lutengano kijiji cha Ushirika Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, John Merina, alithibitisha kutokea kwa vifo hivyo na kueleza majeruhi watatu wamekimbizwa hospitali ya rufaa ya Mbeya kwa ajili ya matibu zaidi.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/17/watu-wawili-wamefariki-katika-ajali-ya-basi-na-kujeruhi-28/

No comments:

Post a Comment