Friday, July 17, 2020

Heche: OCD unahitaji majina ya watia nia Chadema ili iweje?

Aliyekuwa Mbunge wa Tarime vijijini (Chadema), John Heche,  ametoa povu kwa jeshi la polisi kuhusiana na sakata la kutaka majina ya wagombea katika Wilaya ya Nzega.

“Ujinga wa kiwango cha juu, udhalilishaji wa jeshi la polisi .. OCD unaomba majina ya watia nia Chadema ili iweje?,” alihoji Heche.

Heche aliandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa Twitter kuwa “Hii nchi tunahitaji mabadiliko haraka sana,”.

Mkuu wa polisi wa Wilaya ya Nzega amewaandikia barua Chadema ya kuwataka kuwasilisha majina ya watia nia katika majimbo ya Nzega mjini, Nzega vijijini na Bukene.

Barua hiyo ilieleza hivi “Naomba kupatiwa majina ya watia nia kupitia chama cha Chadema kwa majimbo ya Nzega mjini, Nzega vijijini na Bukene majina hayo niyapate kabla ya tarehe 15/07/2020 kwa hatua zangu,”.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/17/heche-ocd-unahitaji-majina-ya-watia-nia-chadema-ili-iweje/

No comments:

Post a Comment