Friday, July 17, 2020

Membe akubali ombi la kugombea urais ajipanga kukutana na Chadema

Mwanachama mpya wa Chama cha ACT-Wazalendo, Bernard Membe amekubali ombi la kugombea urais kupitia chama hicho.

“Jana niliombwa na leo nimekubali rasmi kugombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya chama cha ACT-Wazalendo,” Membe aliandika ujumbe huo kupitia ukurasa wake wa Twitter leo.

Membe ambaye alishawahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje amesema huu ni wakati muafaka kwake kushiriki katika mazungumzo na vyama vingine kama Chadema ili ‘Tusimamishe KISIKI CHA MPINGO’ kimoja!,”.

Membe amejiunga rasmi na chama cha ACT-Wazalendo ambapo wanachama walimuomba agombee urais wakati alipokutana nao jana mlimani City jijini Dar es Salaam.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/17/membe-akubali-ombi-la-kugombea-urais-ajipanga-kukutana-na-chadema/

No comments:

Post a Comment