Monday, July 20, 2020

Bashe,Lukuvi, Talimba Wapeta Kura Za Maoni Ubunge

ImageKada wa chama cha mapinduzi (CCM) Abbasi Talimba ameshinda kwenye kura za maoni za kuwania kuchaguliwa kuwa kupepelesha bendera ya chama hicho kwenye nafsi ya ubunge wa jimbo la kiniondoni mapema mwenzi Oktoba 2020.

Kwenye mchakato huo ulifanywa na wajumbe 492 wa chama hicho wilayani hapo Talimba ameshika nafasi ya kwanza kwa kupata jumla kura 171, akifuatiwa na aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo hili Idd Azzan aliyepata kura 70 bado kura zinaendelea kuhesabiwa.

Kuwa upande mwigine Waziri wa Aridhi William Lukuvi ameshinda zoezi hilo kwenye jimbo la Isimani mkoani Iringa kwa kupata kura 453 kati ya kura 487.

Pia naibu Waziri wa Kilimo Hussen Bashe anayeomba kupitishw ana chama chake kupitia jimbo la Nzega Mjini kwa kushinda kwa kura 367 akiwashinda wagombea wengine 12 waliojitokeza kwenye mchakato huo.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/20/bashelukuvi-talimba-wapeta-kura-za-maoni-ubunge/

No comments:

Post a Comment