Wanafunzi tisa pamoja na walimu nane wamepatikana na virusi vya corona katika shule ya St. Andrews Turi
Wanafunzi hao ambao wote ni raia wa kigeni wamekuwa wakiishi shuleni tangu mwezi Machi
Shule hiyo ilianza maandalizi ya usafiri baada ya rais Uhuru kutoa marufuku ya usafiri wa ndege
Nchi ya Kenya imepata pigo nyingine kuu huku zaidi ya wanafunzi na walimu 17 wa shule moja wakipatikana na virusi vya corona.
Kwa mujibu wa jarida la Standard, wanafunzi hao ambao wote ni raia wa kigeni walilazimika kuishi shuleni humo kwa zaidi ya miezi mitatu tangu kulipuka virusi vya corona, hii ni kufuatia marufuku ya usafiri wa ndege nje na ndani ya Kenya iliyotolewa na Rais Uhuru Kenyatta.
Wanafunzi hao ambao sasa walikuwa katika harakati za maandalizi ya kusafiri hadi nchi zao sasa watalazimika kusalia nchini kupata matibabu pamoja na walimu wao.
Rais Uhuru aliondoa marufu wa usafiri, usafiri wa ndege ukitarajiwa kuanza Julai 15.
source http://www.bongoleo.com/2020/07/10/wanafunzi-na-walimu-17-wa-shule-ya-kifahari-kenya-wapatikana-covid19/
No comments:
Post a Comment