Kikao cha Halmashauri kuu ya kimemchagua rasmi Dk. Hussein mwinyi kuwa mgombea urais wa Zanzibar kupitia CCM.
Kati ya wagombea 32, Mwinyi amepata jumla ya Kura 129 sawa na asilimia 78.65.
Akimtambulisha Rasmi Dk. Mwinyi kwenye kikao hicho, Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais John Pombe magufuli amesema.
“Kwa hiari yenu, kwa mapenzi yenu,kwa moyo wenu na kwa maendeleo ya Chama chenu na taifa lenu kwa kumtanguliza Mungu wenu. Kwa matokeo haya ya kura zilizopigwa na kikao hichi cha Halmashauri kuu ya CCM, Dk. Hussein Mwinyi anakuwa ni mgombea rasmi wa urais Zanzibar kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi.
Kwa upande wake Dkt. Mwinyi amesema
“Kwa sasa hakuna tena Timu Mwinyi wala timu nani, wote ni wamoja na tufanye kazi kwa pamoja. Huu ni mtihani mgumu sana kuwahi kuufanya kwenye maisha yangu, lakini nawashukuru sana.” alisema Mwinyi.
source http://www.bongoleo.com/2020/07/10/dk-mwinyi-atangazwa-kugombea-urais-zanzibar-apata-kura-129/
No comments:
Post a Comment