Mwanamke mmoja raia wa Togo aliyetambulika kama Elizabeth Packal hatimaye amejifungua baada ya kuwa mja mzito kwa zaidi ya miaka kumi.
Inadaiwa kuwa mwanamke huyo anayeishi katika eneo la Oyo alijifungua mtoto wa kike
Ameshindwa kueleza ni nani baba ya mwanawe hadi sasa
Elizabeth ambaye anaishi katika kijiji cha Eiyeosoka, katika wilaya ya Atisbo jimbo la Oyo alijifungua Machi 20, 2020 katika zahanati ya Tayo.
Daktari mkuu katika hospitali hiyo Okawoyin David alieleza kuwa mamake Elizabeth alieleza kuhusu hali ya mwanawe iliyomsumbua kwa miaka kadhaa asiweze kujifungua mtoto.
Alieleza kuwa alipata kuelewa hali hiyo baaa ya kuzunguka naye katika mahospitali kadha wa kadha.
Kulingana na daktari huyo, Elizabeth alikuwa akiugua fibroids. Hii ni kwasabau hata baada ya kujifungua, tumbo lake lilisalia limefura kama anayetarajia mtoto mwengine.
Licha ya Elizabeth kudai kuwa amekuwa na mimba kwa zaidi ya miaka kumi, daktari ameeleza kuwa hali hiyo haina maelezo. Amesisitiza kuwa mama huyo hakuweza kupata mimba hapo awali kutoka na shida ya uzazi na punde baada ya kutibiwa aliweza kupata ujauzito na hatimaye kujifungua mtoto wa kike.
Kuzaliwa kwa mtoto huyu kulimpa Elizabeth furaha isiyo kifani licha ya kuchanganyikiwa kuhusu baba wa mtoto huyo. Kulingana naye, hawezi kujua baba wa mtoto huyu maana amekuwa na ujauzito kwa muda mrefu.
source http://www.bongoleo.com/2020/07/10/mwanamke-ajifungua-baada-ya-kuwa-mja-mzito-kwa-miaka-10/
No comments:
Post a Comment