Wednesday, July 15, 2020

Wanafunzi 55 Waambukizwa Corona Huku Shule Zikifunguliwa Ghana

Coronavirus Exacerbates Islamophobia in India | Time

Wafanyikazi wengine 314 wametiwa karantini baada ya kupatikana na virusi vya corona. Picha: Hisani

Wanafunzi 55 pamoja na walimu wengine wa shule moja ya upili nchini Ghana wameambukizwa virusi vya corona

Kwa mujibu wa wizara ya afya wa nchi hiyo, wafanyikazi wengine 314 wametiwa karantini baada ya kupatikana na virusi vya corona.

Kulingana na ripoti hiyo, imebainika kuwa wanafunzi hao ambao wengi walikuwa watahiniwa walirejea shuleni kujitayarisha kwa mtihani mkuu wa kitaifa.

Kisa cha kwanza cha maambukizi ya virusi vya corona kiliripotiwa shuleni humo wiki jana kabla visa hivyo kupanda hadi 54 baadaye wiki hii.

Fifty-five students have been diagnosed with COVID-19 virus after a school opened in Ghana

Kwingineko, Rais Nana Akufo alilazimika kujifungia kwenye jela kwa siku 14 baada ya kutangamana na waathiriwa wa virusi vya corona.

Idadi ya watu waliambukizwa virusi vya corona imezidi kuongezeka,  shirika la afya duniani WHO ikitoa onyo kali. Kulingana na shirika hilo, idadi ya maambukizi itaongezeka maraduf iwapo mataifa yatazidi kukiuka kanuni zilizowekwa na shirika hilo.

Aidha shirika hilo limeonya dhidi ya kufungua shule, likisema kuwa hiyo itakuwa njia ya kuhatarisha maisha wanfunzi.

Wameshauriwa kusubiri hadi makali ya virusi vya corona kupunguka kabla kufunguliwa shule hizo.

Hadi sasa takriban watu 13, 249,575 wameambukizwa virusi vya corona duaniani na zaidi ya vifo nusu milioni.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/15/wanafunzi-55-waambukizwa-corona-huku-shule-zikifunguliwa-ghana/

No comments:

Post a Comment