Thursday, July 16, 2020

Wanachama ACT Wamuomba Membe Achukue Fomu ya Urais

ImageMwenyekiti wa chama cha ACT-WazalendoMaalim seif Hamad amemuomba aliyekuwa waziri wa mambo ya nje na mwananchama mpya wa chama hicho Bernard Membe kutimiza maombi ya wanachama wa chama hicho ya kuchukua fomu ya urais.

Akizungumza wakati wa kumtambulisha rasmi Membe kwa wanachama wa ACT Maalim Seif amesema ujio wa Membe utaongeza kiasi kikubwa umaarufu wa chama hicho duniani kote.

“Membe ni maarufu nchini na Dunia inamtambua, chama chetu kama kilikuwa kinajulikana Kenya na Uganda sasa kinajulikana Dunia nzima, Membe wamekusikia lakini wanachama wanakuomba uchukue fomu ya kugombea Urais, hata ukipenda chukua leo leo” amesema Maalim.

Ikumbukwe Bernard Membe alifukuzwa ndnai ya chaa chake cha awali (CCM) kutokana na kutangaz ania ya kugombea urais kupitia chama hicho kwenye uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi oktoba mwaka huu.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/16/wanachama-act-wamuomba-membe-achukue-fomu-ya-urais/

No comments:

Post a Comment