Thursday, July 16, 2020

Naibu Chifu Mashakani, Afumaniwa Ana kwa Ana Akimbaka Mwanafunzi Msituni

Deputy Chief, police disappear after allegedly raping a Form 3 girl

Wenyeji hao waliweza kumkamata naibu chifu mmoja huku washukuwa wenzakake wakipotea msituni mbio. Picha: Hisani.

Maafisa wa polisi wamemkamata naibu chifu na kuanza msako mkali dhidi ya polisi mmoja baada ya kudaiwa kushirikiana katika kumnajisi mwanafunzi mmoja msituni.

Watatu hao walifumaniwa na wenyeji waliojawa ghadhabu katika msitu mmoja Jumatano, Julai 15 kama ilivyoripotiwa na jarida la Citizen.

Machifu hao wawili, momja kutoka Tuthu na mwengne Wanjere walishirikiana na afisa mmoja wa polisi walimakamata msichana huyo wa kidato cha tatu na kumpeleka hadi msitu wa Abedare kabla kuanza kummnajisi.

Inadaiwa kuwa mzee mmoja aliwaona watatu hao wakiandamana na msichana huyo msituni na ndipo akaenda upesi kuwajuza wenyeji ambao walianza kuwasaka muda mfupi baadaye.

Wenyeji hao waliweza kumkamata naibu chifu mmoja huku washukuwa wenzakake wakipotea msituni mbio.

Kamanda wa polisi wa eneo hilo John Ngare alithibitisha kisa hicho akieleza kuwa maafisa wake wameanzisha msako mkali dhidi ya wawili waliotoroka.

Visa vya unajisi hawa wa watotowa shule vimezidi kupanda haswa tangu kulipuka virusi vya corona huku idadi wa  wanfunzo wanaopachikwa mimba ikiongezeka maradufu.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/16/naibu-chifu-mashakani-afumaniwa-ana-kwa-ana-akimbaka-mwanafunzi-msituni/

No comments:

Post a Comment