Thursday, July 16, 2020

Wahudumu wa Afya Wasusia Kazi Baada ya Wenzao Kuambukizwa Covid19

Bahari FM.

Wauguzi hao walilalamikia usalama wao haswa baada ya wenzao sita kuambukizwa. Picha: Hisani

Wahudumu hao wa afya walilalamika kuhusu jinsi serikali ya kaunti ilivyodinda kuwapa vifaa salama vya kujikinga

Walidai kuwa wenzao sita walikuwa wameambukizwa virusi vya corona na kuwa maisha yao vile vile yamo hatarini

Shughuli za matibabu zililemazwa katika hospitali ya King Fahad katika kaunti ya Lamu, Kenya huku wahudumu wa afya wakisusia kazi.

Wauguzi hao walilalamikia usalama wao haswa baada ya wenzao sita kuambukizwa virusi hatari vya corona siku chache zilizopita.

Wahudumu wa afya hao waliokuwa wakigoma wametishia kulemaza shughuli nyingi zaidi haswa wakilalamika kuwa serikali ya kaunti hiyo imewapuuza na kudinda kuangazia usalama wao kazini.

Kulingana nao, wenzao waliothibitishwa kuambukizwa virusi hivyo walikuwa katika hatari kubwa kutokana na kutokuwepo vifaa mwafaka vya kujikinga na virusi hivyo wakati wakuwahudumia waathiriwa.

Katibu wa muungano wa kutetea haki za wauguzi Kenya, Alfred Obengo aliikashifu hospitali hiyo kwa kile alichokitaja kama utepevu kuhusiana na usalama wawauguzi.

‘’ Hatuwezi kuilaumu serikali na waziri wa afya kwa kuwatuma wahudumu wa afya katika maneo hatari.  Lawama hapa ni kwa usimamizi maeneo yaliyoathorika,’’ Obengo alisema.

Serikali ya Kenya ilithibitisha kuwa wahudumu afya 429 walikuwa wameambukizwa virusi hivyo hatari hadi Jumanne, Julai 14.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/16/wahudumu-wa-afya-wasusia-kazi-baada-ya-wenzao-kuambukizwa-covid19/

No comments:

Post a Comment