Thursday, July 16, 2020

Manara: Hatutofanya Usajili Mkubwa

FA Cup: If Simba SC lose to Yanga SC I will give Nugaz, Bumbuli ...Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara amesema timu hiyo haitofanya usajili mkubwa kwenye dirisha kubwa la usajili baada ya kukamilika kwa msimu ujao wa ligi kuu bara kwa lengo la kuimalisha zaidi kikosi chao.

Akizungumza kwenye mahojiano na kituo cha Wasafi FM amesema watafanya usajili mdogo kwenye maeneo yenye upungufu tu na sio kusajili kila mchezaji kwa namna ambayo sio nzuri kwa timu hiyo inayojianda kushiriki michuano ya klabu bingwa afrika.

“Usajili wa msimu ujao tusajili kwenye maeneo maalum tu kikosi hakitakuwa na mabadiliko makubwa. Tunaweza kusajili mabeki wawili na washambuliaji wawili” amesema Manara.

Ikumbukwe kalbu ya Simba imeshachukua buningwa wa ligi kuu bara hali inayowapa uwezowa kushirikia ligi kwenye michuano ya klabu bingwa barani afrika michuano yenye heshima na thamani zaida ngazi ya vilabu barani afrika.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/16/manara-hatutofanya-usajili-mkubwa/

No comments:

Post a Comment