Thursday, July 16, 2020

Wagombea CCM Wafika 8000 Dar, Arusha Vinara

CCM Presidential Candidate Dr. John Magufuli Proclaimed New ...Rais John Magufuli ameweka wazi kuwa mpaka kufikia leo julai 16, 2020 Alfajili kulikuwa na jumla ya wagombea 8205 kupita chama cha mapinduzi (CCM) walikichukua fomu za kuomba kuteuliwa kwenye nyadhifa mbalimbali kwenye uchaguzi ujao.

Akizunguzma lkulu Chamwino jijini Dodoma amesema hatua hiyo inaonyesha ni namna gani chama cha mapinduzi kinavyoonesha kukubalika na wananchi kiasi cha kuvutia wananchama wengi kwenda kuchukua fomu.

“Mpaka kufikia leo Alfajili niliambiwa kuwa kuna watu 8205 waliojitokeza kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa ndani ya CCM na nasikia Dar es salaam ndiyo inaongoza kwa watinia mpaka napewa taarifa walikuwa 839, Arusha wapo 820 Kagera 328 hii inaonyesha namna gani chama chetu kinavyokubalika, ndugu zangu kafanyeni kazi” amesema Rais Magufuli.

Ikumbukwe kuwa chama cha mapinduzi kimefungua ramsi zoezi la kuanza kuchukia fomu za kuomba kuteulia ndani ya chama kuelekea kwenye uchaguzi wa wabunge,madiwani na wawakilishi mapema mwenzi Oktoba.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/16/wagombea-ccm-wafika-8000-dar-arusha-vinara/

No comments:

Post a Comment