Thursday, July 16, 2020

Rais Magufuli amesema idadi ya waliotangaza kugombea hadi leo wamefikia 8,000 na Dar inaongoza

Rais John Magufuli amesema amepata taarifa ambao wametangaza kugombea mpaka leo ni zaidi ya 8,000.

Rais Magufuli amesema hayo leo wakati akiwaapisha wateule Ikuku jijini Dodoma.

Magufuli amesema mkoa wa Dar es Salaam ndio unaongoza mpaka asubuhi watu 829 wametangaza nia.

“Nilikuwa napewa taarifa hapa na Makamu wa Rais waliojitokeza kutia nia kupitia CCM mpaka sasa ni zaidi ya 8000 na Dar es Salaam ndiyo inaongoza ambayo mpaka Leo alfajiri wapo 829,” amesema Magufuli.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/16/rais-magufuli-amesema-idadi-ya-waliotangaza-kugombea-hadi-leo-wamefikia-8000-na-dar-inaongoza/

No comments:

Post a Comment