Thursday, July 16, 2020

Mpishi wa Pombe Haramu Avunja Gari la Polisi Makusudi, Akataa Asikamatwe

Police-Lorry

David Ongweno Nambwaya alishtakiwa kwa kosa la kuzua vurugu na kulivunja kioo. Picha: Hisani

Jamaa mwenye umri wa makamo alishtakiwa Jumatano, Julai 15 baada ya kudaiwa kuvunja kioo cha gari la polisi katika mtaa wa Embakasi, Nairobi akivurugana na maafisa hao wasimkamate.

David Ongweno Nambwaya alishtakiwa kwa kosa la kuzua vurugu na kulivunja kioo hicho makusudi baada ya mkewe pamoja na walevi wengine kuzingirwa na polisi wakiandaa na kubugia kileo haramu cha Chang’aa.

Kisa hicho kilifanyika Jumapili wakati maafisa wa kituo cha Soweto wakiongozwa na Inspekta Wilson Kaguru walipoandamana katika oparesheni ya kuwakamata wapishi na wabugiaji wa pombe haramu.

Kenya's deadly illegal spirit – changaa – Africa Sustainable ...

Jamaa akiandaa pombe haramu ya chang’aa. Picha: Hisani.

Walipofika katika boma ya Nambwaya, maafisa waliwazingira kundi la wabugiaji pombe hiyo akiwemo mkewe, Wambui Ndungu.

Katika harakati ya kuwaelekeza katika lori ya polisi,  jama huyo pamoja na wenzake walizua fujo na kuanza kulinyeshea gari la polisi mawe.

Maafisa hao walilazimika kufyatua marisasi hewani kuwatawanya walevi hao waliojaribu kulichoma gari lao.

Maafisa hao walilazimika kuondoka hapo na kurudi siku tatu baadaye na kumkamata Nambwaya ambaye kwa wakati huo alipatikana na lita mbili ya pombe hiyo haramu ya chang’aa.

Alifikishwa katika mahakama ya Makadara alikokataa mashtaka na kuachiliwa kwa dhamana ya KSh 15, 000 kesi hiyo ikitarajiwa kutajwa tena Novemba 20.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/16/mpishi-wa-pombe-haramu-avunja-gari-la-polisi-makusudi-akataa-asikamatwe/

No comments:

Post a Comment