Wednesday, July 15, 2020

TMA imetoa tahadhari ya kuwepo kwa hali mbaya ya hewa kwa siku tano

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) imetoa tahadhari ya kuwepo kwa hali mbaya ya hewa kwa siku tano.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo katika vyombo vya habari imeeleza kuwa leo Julai 15, 2020 kutakuwa na upepo mkali unaofika kilometa 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofika mita mbili.

“Baadhi ya maeneo ya ukanda wa Pwani ya Bahari ya Hindi, mikoa ya Lindi, Mtwara, Tanga, Dar es Salaam na Pwani ikujumlishwa na visiwa vya Mafia na visiwa vya Unguja na Pemba,”.

TMA imeeleza kiwango cha athari zinazoweza kutokea ni wastani katika kuathiri kwa baadhi ya shughuli za uvuvi.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Julai 16, 2020 kutakuwa na taadhari kubwa ya upepo mkali unaofikia kilometa 60 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofika 3.5 ambayo imetolewa kwa maeneo ya Ukanda wa Pwani ya Bahari ya Hindi, Mtwara, Dar es Salaam, Pwani, visiwa vya Pwani , Tanga na visiwa vya Unguja na Pemba.

TMA imeeleza kuwa Julai 17, 2020 kutakuwa na upepo mkali unaofika kilometa kilometa 60 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofika 3.5 ambayo imetolewa kwa maeneo ya Ukanda wa Pwani ya Bahari ya Hindi, Mtwara, Dar es Salaam, Pwani, visiwa vya Pwani , Tanga na visiwa vya Unguja na Pemba.

Imeeleza kuwa kiwango cha arhari ambacho kinaweza kutokawa kwa Julai 16 na 17 ni kikubwa na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari.

Jumamosi ya Julai 18, 2020 TMA imetoa tahadhari ya upepo mkali unaofika kiwango cha kilometa 50 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofika 3.0. Imetolewa kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa Pwani ya Bahari ya Hindi (mkoa wa Lindi, Mtwara, Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Visiwa vya Mafia na Unguja na Pemba.

TMA imeeleza kuwa Jumapili ya Julai 19, 2020 kutakuwa na upepo mkali unaofika kilometa 50 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofika 2.5 imetolewa kwa baadhi ya maeneo ya Ukanda wa Bahari ya Hindi (Mikoa ya Lindi, Mtwara, Dar es Salaam, Tanga na Pwani, visiwa vya Mafia pamoja na visiwa vya unguja na Pemba.

“Athari zinazoweza kujitokeza ni kuathiri kwa baadhi ya shughuli za uvvuvi na usafirishaji pamoja na kuezuliwa kwa baadhi ya paa zisizo imara,” ilieleza taarida hiyo.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/15/tma-imetoa-tahadhari-ya-kuwepo-kwa-hali-mbaya-ya-hewa-kwa-siku-tano/

No comments:

Post a Comment