Wednesday, July 15, 2020

Rais Magufuli awatumbua wakuu wa mikoa akiwemo Makonda

Rais John Magufuli amefanya uteuzi wa viongozi wa mikoa na wilaya na kumteua Abubakar Kunenge kuwa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam.

Kabla ya uteuzi huo Kunenga alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam na anachukua nafasi ya Paul Makonda.

Rais Magufuli amemteua Joseph Joseph Mkirikiti kuwa mkuu wa mkoa Manyara . Kabla ya uteuzi huo Mkirikiti alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Hanang  mkoani Manyara  na anachukua nafasi ya Alexander Mnyeti.

Rais Magufuli amemteua Paulo Mshimo Makanza kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam.

Kabla ya uteuzi huo Makanza alikuwa Ofisa Mwandamizi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) anakwenda kuchukua nafasi ya Aboubakar Kunenge ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Rais Magufuli amemteua Dk. Seleman Serera kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma.

Kabla ya uteuzi huo Dk Serera alikuwa Ofisa Mwandamiza wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Makao Makuu na anachukua nafasi ya Deo Ndejembi.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/15/rais-magufuli-awatumbua-wakuu-wa-mikoa-akiwemo-makonda/

No comments:

Post a Comment