Wednesday, July 15, 2020

Pasta Maarufu Aliyeambukizwa Covid19 Apona Ghafla

I partied hard but did not drink, says Burale

Burale  aliwekwa katika ICU kwa muda wa wiki moja. Picha: Hisani

Mtumishi maarufu nchini Kenya Robert Burale ameripotiwa kupona na kuondoka hospitalini wiki moja baada ya kuripotiwa kuambukizwa virusi hatari vya corona.

Burale ambaye wengi walishuku ukweli kuhusu kuambukizwa virusi hivyo aliwekwa katika ICU kwa muda wa wiki moja.

Mmoja wa rafiki zake ambaye alichapisha ujumbe kuhusu kutoka kwake hospitalini alieleza kuwa mhubiri huyo sasa anaendelea kupata nafuu nyumbani kwake katika mtaa wa Karen.

View this post on Instagram

@burale1 beats Covid

A post shared by Urban News (@urbannews254) on

‘’ Robert Burale yuko nyumbani kwake.  Nawashukuru wale wote waliomuombea,’’ Nina Njoroge aliandika.

Si huyo tu, mhubiri mwenza aliteyambulika kama Karol Tunduli alithibitisha kuwa Burale alikuwa nyumbani huku akionyesha furaha yake kuhusu kupona kwa mchungaji huyo.

Now we can talk and laugh at your new name when CS Kagwe called you Robert Murathe !Welcome home sir 🙏 🙌 ☺ We will keep praising through the battle wonIsrael Robert Burale

Posted by Karol Tunduli KtSnr on Tuesday, 14 July 2020

Sasa tunaweza kucheka kuhusu jinsi waziri wa afya alivyokupa jina jipya alipokuita Robert Murathe. Karibu nyumbani. Tutazidi kumshukuru sana kwa ushindi wako Robert Burale,’’ alisema Tunduli.

Burale alipatwa na virusi hivyo na kujirusha mtandaoni kuwatadharisha wengi wa Wakenya waliokuw wakishuku kuhusu kuwepo virusi hivyo, baadhi wakidai kuwa hiyo ilikuwa ni kuagiza tu.

‘’ Nlipimwa na kupatikana na virusi vya corona saa 24 baadaye.  Daktari huyo alikuja katika chumba nilimokuwa na kujijuza kuwa nilikuwa nikiugua corona na hivyo singerudi nyumbani,’ alisema.

Wengi walishuku uhalisia wa maambukizi yake haswa baada ya kubainika kuwa alifanya video hiyo hata alipokuwa katika ICU.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/15/pasta-maarufu-aliyeambukizwa-covid19-apona-ghafla/

No comments:

Post a Comment