Hafiz Rahim Afariki. Picha:Hisani.
Hafiz Rahim, aliyekuwa mshambulizi wa timu ya kitaifa ya Singapore amefariki
Nyota huyo alifariki akiwa na umri wa miaka 36 baada ya kuhusika katika ajali mbaya ya barabara
Rahim ameacha nyuma mjane pamoja na wanawe
Aliyekuwa mshambulizi sugu wa timu ya kitaifa ya Singapore Hafiz Rahim ameripotiwa kufariki akiwa na umri wa miaka 36.
Nyota huyo mstaafu wa kandanda alipoteza maisha kufuatia ajali mbaya barabara alipokuwa akiendesha pikipiki katika eneo la Tampiness, hii ni kwa mujibu wa jarida la The straight Times.
Rahim ambaye aliichezea klabu ya Tampiness Rovers kwa mara ya mwisho kabla kustaafu ameacha nyuma mjane pamoja na wanawe.
Hafiz alianza kandanda ya kulipwa kwa kuichezea timu ya kitaifa ya Singapore 2004 kabla kujiunga na Gombak United, Home United na hatimaye Warriors.
The FAS is deeply saddened to learn about the passing of Hafiz Rahim. A skilful attacker, he scored the goals that won Geylang's 2011 Singapore Cup and Warriors' 2014 S.LEAGUE.
Our thoughts and condolences go out to Hafiz's family and loved ones during this difficult time. #SPL pic.twitter.com/oiPG85oPDt
— Singapore Premier League (at ) (@SGPremierLeague) July 9, 2020
Aliichezea Singapore mara tisa kutoka 2011 hadi 2020 na kufunga bao moja.
Hafiz aliifungia klabu ya Geyland bao la ushindi katika mashindano ya finali za 2009 Singapore.
Watu wa kila tabaka wamemkumbuka nyota huyu kwa jumbe kadhaa za rambirambi.
We are shocked and saddened to learn about the death of our former Stag, Hafiz Rahim from a traffic accident. We wish to extend our deepest sympathy and condolences to Hafiz's family and friends. pic.twitter.com/ZnvLOyXeG2
— Tampines Rovers FC (@TRFCStags) July 9, 2020
source http://www.bongoleo.com/2020/07/10/tanzia-aliyekuwa-mshambulizi-wa-singapore-hafiz-rahim-afariki/
No comments:
Post a Comment