Friday, July 10, 2020

Msafara wa Catherine Ruge akirejesha fomu ya ubunge wapigwa mabomu

Msafara wa aliyekuwa mbunge wa viti maalum (Chadema), Catherine Ruge mkoani Mara amezuiliwa kwa kupigwa mabomu na jeshi la polisi.

Mabomu hayo yalianza kurindima wakati akirejesha fomu ya kuwania Ubunge jimbo la Serengeti kupitia Chadema.

Licha ya kupigwa mabomu ya machozi Catherine Ruge alifanikiwa kurejesha fomu yake ya kugombea ubunge.

Ruge  awajibu polisi “Polisi kaeni pembeni tuacheni huu mziki na CCM,” aliandika katika ukurasa wake wa twitter.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/10/msafara-wa-catherine-ruge-akirejesha-fomu-ya-ubunge-wapigwa-mabomu/

No comments:

Post a Comment