Tuesday, July 14, 2020

Shilole Afunguka Kuhusu Uchebe “Maisha Yanaendelea”

Shilole + Uchebe = Mapacha wa Mwendokasi – Eposite | EpodigitalIkiwa imepita takribani siku tano tangu mwanamuziki Zuena Mohamed (Shilole) kutuma ujumbe kwenye ukurasa wake wa instagram akidai amepigwa na aliyekuwa mume wake Ashrafu Sadiki (Uchebe) hatimaye amefunguka rasmi juu ya maendeleo yake baada ya tukio hilo.

Kupitia ujumbe alituma kwenye ukurasa wake wa instagram Shilole amesema anaendelea vizuri na amewashukuru watanzania waliomuombea kipindi alipokuwa anapitia kwenye matatizo hayo.

“Maisha yanaendelea, tuendelee kuijenga jamii yetu, Jamii itakayokataa kabisa unyanyasaji wa kijinsia, Kuhusu maendeleo yangu mimi niko sawa, naendelea kupambana, changamoto ni sehemu ya maisha, haziwezi kunifanya nianguke, lakini yote hayo sio kwa nguvu zangu, ni Mungu na upendo wa Watanzania wenzangu mnaonitakia mema” ameandika Shilole.

Ikumbukwe mapema Julai 9, 2020 mwanamuzki huyo alitangaza kuachana na mume wake huyo baada ya kitendo cha kupingwa na kujeruhiwa kutokan na sababu alizozitaja kuwa ni migogoro ya ndoa.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/14/shilole-afunguka-kuhusu-uchebe-maisha-yanaendelea/

No comments:

Post a Comment