Tuesday, July 14, 2020

Askofu wa Miaka 68 Aliyempokonya Bwana Harusi Mke Auawa Kinyama

bishop 1

Mwaka jana askofu Francis Mugweru aligonga vichwa  vya habari si kwa kuhubiri injili bali kwa kumpokonya jamaa mkewe na kumuoa rasmi.

Inaidawa kuwa Askofu huyo ambaye ni kiongozi wa kanisa la Joyspring Soul Winning alimshawishi mwanamke huyo na kutoroka naye hata baada ya kumuunganisha rasmi na mumewe kwa njia ya harusi.

Mwili wa askofu huyu ulipatikana asubuhi ya Jumanne, 14 Julai katika msitu mmoja karibu na nyumbani kwake ukiwa na majeraha mabaya.

Aidha, inadaiwa kuwa askofu huyo alitolewa na wauaji wake usiku na kupigwa hadi kifo kabla ya mwili wake kutupwa katika msitu huo.

Samwel Njuguna ambaye ni nduguye mwendazake ameitaka polisi kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua wauaji wa nduguye.

‘’ Tunataka haki itendeke kwa ndugu yetu, ambaye pia ni kiongozi wetu wa kiiimani, polisi wasipumzike hadi wauaji wapatikane,’’ alisema.

Kulingana na Njuguna, aliupita mwili huo karibu na njia akielekea kazini ila hakumtambua kama ndugu yake

‘’ Niliuona mwili nikiwa njiani kuenda kazini Thika lakini sikumtambua. Saa moja baadaye, nilipiwa simu na majirani kuambiwa kuwa aliuliwa,’’ Njuguna aliongezea.

Waumini wa kanisa la askofu huyo wakiongozwa na kasisi Lincoln Mwaniki  wamemtaja kama mtumishi wa Mungu mtiifu ambaye alifanya kazi kubwa katika kufungua makanisa kadhaa katika eneo hilo.

bishop 3

Inadaiwa kuwa askofu huyo alikosana na mkewe manamo 2013 baada ya kuishi naye kwa miaka 34 na kujaliwa watoto watatu pamoja.

Mtumishi wa Mungu alipata nafasi ya kupata mke wa pili, wakati huu akimpokonya muumini wake baada ya kuwafunganisha kwa harusi.

Mume wa mwanmke huyo aliingiwa na hasira baada ya mtumishi wa Mungu kumpokonya mke na kumkodishia anyumba na hata kuahidi kumfanyia masihara.

Mwili wa marehemu ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha  Kago Genereal Thika huku uchunguzi ukianzishwa kubaini chanzo cha kifo chake.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/14/askofu-wa-miaka-68-aliyempokonya-bwana-harusi-mke-auawa-kinyama/

No comments:

Post a Comment