Thursday, July 16, 2020

RC Mbeya Atoa Sababu Za Kubadilia Gia Angani.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila aagiza mawakala mashine za ...Mkuu wa mkoa wa Mbeya Albert Chalamila ametoa sababu tatu kubwa zilizofanya ashindwe kwenda kugombea ubungewa jimbo la Iringa mjini kama alivyotangaza nia hapo awali.

Akuzungumza leo Julai 16, 2020 wakati wa hafla ya kuwaapisha viongozi mbalimbali walioteuliwa na Rais John Magufuli hivi karibuni Ikulu Chamwino jijini Dodoma amesema alibadili mambo hayo kutokana na ushauri alioutoa Rais Magufuli.

“Mimi mpaka animebewa jina ninaitwa mzee wa “U turn” na magazeti yaka andika kuwa nimebadili gia angani lakini ngoja niseme kuwa nilifanya vile baada ya mimi baada ya kuona maendeleo, kuangalia umeleta zaidi ya bilioni 3 za kurakabati miundombinu ya elimu pale Mbeya, umeleta pesa kwa ajili ya kujenga vituo vya afya Mbeya nzima sasa  nikajiuliza mimi nikiondoka nani atasimamia haya mambo ndio maan nilamua kubaki Mbeya” amesema.   

Ikumbukwe kuwa mapema mwezi Juni mkuu huyo wa mkoa alitangaza nia ya kugombe aubunge kwenye jimbo la Iringa mjini lakini alibadilia nia yake hiyo bada ya hotua ya Rais juu ya watumishi waotaka kugombea kwenye uchaguzi ujao.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/16/rc-mbeya-atoa-sababu-za-kubadilia-gia-angani/

No comments:

Post a Comment