Habari ya asubuhi mdau wa Opera News ni siku nyingine ya Alhamisi Julai 16, 2020, matumaini yetu upo salama na karibu katika ujenzi wa taifa.
Tunakukaribusha katika dawati letu la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazopamba asubuhi ya leo.
Habari hizo ni Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe asema Sheikh Ponda haonekani kwenye vituo vya polisi kulikoni? Mume amuua mkewe kwa kumchinja shingoni na yeye kujinyonga je unajua chanzo cha kutokea mauaji hayo ni nini? soma habari hii kwa kina na matokeo kura za maoni Chadema yashtua wengi.
Karibu msomaji wetu;
ZITTO: NIMEJULISHWA NA MAWAKILI SHEIKH PONDA HAONEKANI KATIKA VITUO VYA POLISI
Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema amejulishwa na mawakili kuwa Sheikh Ponda Issa Ponda haonekani kwenye vituo vyote vya polisi jijini Dar es Salaam.
“Pamoja na juhudi zinazofanywa na mawakili kuhakikisha kuwa anafikishwa mahakamani,” aliandika Zitto katika ukurasa wake wa twitter.
Zitto amelitaka jeshi la polisi kumuachia huru mara moja Sheikh Ponda na kwamba wanatakiwa kutenda haki.
MUME AMUUA MKEWE KWA KUMCHINJA SHINGONI NA YEYE KUJINYONGA
Mkazi wa Kijiji cha Mipanga Kata ya Maji Moto Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi, Dalali Malongo (20) ameuawa kikatili kwa kuchinjwa shingo na mume wake aitwaye, Kisabo Joseph baaada ya mume wake kukasirishwa na kitendo cha mke wake kumnyima tendo la ndoa kwa muda mrefu.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Benjamin Kuzaga amesema tukio hilo la mauaji lilitokea Julai 14, mwaka huu majira ya saa moja jioni Kijiji cha Mipanga Kata ya Maji Moto Wilaya ya Mlele.
Amesema marehemu na mtuhumiwa walikuwa ni wanandoa waliokuwa wakiishi pamoja kama mume na mke.
MATOKEO KURA ZA MAONI CHADEMA YASHTUA WENGI
MMATOKEO ya kura za maoni ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), yameendelea kushtua kutokana na makada wanawake wa chama hicho kuibuka washindi katika maeneo mengi.
Katika kura hizo zilizoanza kupigwa mwanzoni mwa wiki, wabunge waliomaliza muda wao katika Bunge lililopita kupitia chama hicho, wameibuka washindi.
Kwa matokeo yaliyotangazwa jana, waliong`ara katika kura za maoni ni Lucy Owenya (Moshi Vijijini) ambaye pia ameshinda kwenye kipengele cha ubunge viti maalum kwenye jimbo hilo hilo.
source http://www.bongoleo.com/2020/07/16/dondoo-za-leo-zitto-asema-sheikh-ponda-haonekani-vituo-vya-polisi-mume-amuua-mkewe-kwa-kumchinja-na-yeye-kujinyonga-na-matokeo-kura-za-maoni-chadema-yashtua-wengi/
No comments:
Post a Comment