Thursday, July 16, 2020

Magufuli : Sijamtuma Mtu Kugombea

Opinion: Tanzania's Magufuli, a reformist or dictator? | Africa ...Rais John Magufuli amesema kuwa hajamtuma mtu yoyote yule kwenda kugombea kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mapema wezi oktoba mwaka huu.

Akizunguzma leo Julai 16, 2020 wakati wa kuwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua Ikulu Chamwino jijini Dodoma, Rais Magufuli amesema kama kuna watiania wanaopita huko kusema mimi nimewatuma ni waongo na wananchi msiwasikilize.

“Hakuna mtu yoyote aliyemtuma na mimi hakuna aliyetumwa na waziri mkuu hakuna aliyetumwa na makamu wa rais kama wapo watu wanazungumza kuwa mimi nimewatuma mimi watie nia jamani hao ni  waongo, sijatuma mtu kama ningekuwa nakutaka si ningekuchagua kwenye vile viti vyangu kumi”amesema Rais magufuli.

Ikumbukwe kuwa Rais John Magufuli amekuwa akisisitiza kuwa hatosita kuwapa ruhusa viongozi wate wanaotaka kugombea kwenye uchaguzo ujao lakini hawezi kuacha nafasi ibaki wazi isubiri kiongozi aliyekwenda kugombea.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/16/magufuli-sijamtuma-mtu-kugombea/

No comments:

Post a Comment