Monday, July 20, 2020

Rais Magufuli: Dk Seif alishawahi kuomba kugombea ubunge Korogwe hakuwa na hela akapigwa chini

 

Rais John Magufuli amesema DK. Seif Shekalagh ni daktari mwenye taaluma na amesoma akapatiwa Shahada ya Udhamivu (PHD) kutoka nchini Uholanzi na kwenda kwenye kituo cha utafiti.

“Miaka ya nyumba aliomba  Ubunge Korogwe  hakuwa na hela wala nini alitaka kuwatumikia wana korogwe akapigwa chini,” amesema Rais Magufuli.

“Alivyokosa ubunge akaurudi kwenye mambo yake ya utafiti alipoondoka nikasema mbona huyu anapenda siasa nikaona acha nimjaribu kidogo,” amesema Rais

Rais Magufuli amesema alimpa nafasio ya ukuu wa wilaya ya Maswa, hakukata tamaa akaenda kufanya kazi vizuri.

“Maswa  ni miongoni mwa Wilaya zilizoanzisha viwanda vya mkakati ndio maana tukasema tumpandishe,” alisema Magufuli



source http://www.bongoleo.com/2020/07/20/rais-magufuli-dk-seif-alishawahi-kuomba-kugombea-ubunge-korogwe-hakuwa-na-hela-akapigwa-chini/

No comments:

Post a Comment