Monday, July 20, 2020

Lionel Messi Avunja Rekodi kwa Mara Nyingine, Atuzwa Kishujaa

Lionel Messi becomes 1st player to create 21 assists in la Liga history

Messi ameibuka mshindi wa mabao, akijizolea takariban mabao 25 katika ligi La Liga. Picha: Hisani.

Lionel Messi ameibuka mshindi licha ya timu yake kufeli kutwaa ushindi wa La Liga

Mshambulizi huyo wa kalabu ya  Barcelona ameibuka mshindi wa mabao, akijizolea takariban mabao 25 katika ligi La Liga

Mwanakandanda hodari wa klabu ya Barcelona Lionel Messi ana sababu ya kutabasamu licha ya timu yake kufeli kutwaa ubingwa katika ligi ya La Liga kwa misimi mitatu mtawalia.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 33 aliibuka mshindi wa mabao kwa kuvunja rekodi ya La Liga baada ya ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Catalans, yeye akijibariki kwa mabao mawili kwenye mechi hiyo.

Messi alimpiku aliyekuwa kocha wake na kuweka rekodi mpya kwa kusaidia katika ushindi wa mabao 21 katika msimu moja.

Kando na Messi na Fati, Luis Suarez na Nelson Semedo walikuwa mpangoni ila Real Madrid ikawapiku.

Raia huyo wa Argentine pia aliweza kumaliza msimu katika nafasi ya mfunga bao bora akiwa na mabao 25 katika mechi 33 na kumpiku Karim Benzema kwa mabao 21.

Licha ya kuvunja rekodi hiyo, Lionel Messi alikuwa na uchungu kwa timu yake iliyokosa kutwaa ushindi wa ligi.

‘’ Hatukutaka kumaliza msimu hivi lakini inaonyesha jinsi msimu ilivyokuwa,’’ alisema.

Tulikuwa na makosa mengi, wanyonge, na bila motisha.  Lazima tujihoji,’’ aliongezea.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/20/lionel-messi-avunja-rekodi-kwa-mara-nyingine-atuzwa-kishujaa/

No comments:

Post a Comment