Monday, July 20, 2020

Diamond na Wema Sepetu Watesa Mitandao kwa Densi ya Mapenzi, Wanarudiana?

Hodari Wa Mapenzi: Diamond and Wema Sepetu spotted dancing suggestively at high-end event

Kampuni maarufu inayomilikiwa na Diamond Platnamaz, Wasafi, iliandaa hafla kumshrehekea msanii mpya Zuchu

Wema na Diamond waliawaacha wengi vinywa wazi kwa densi yao katika hafla hiyo

Walinengua viuno kwa tabasamu na kumbukumbu za mapenzi yao ya zamani

Ni wazi kuwa chembe chembe za mapenzi kati ya Diamond Platnamz na Wema Sepetu zingali zipo na sherehe iliyoandaliwa na kampuni ya Wasafi imethitisha hili.

Wawili hao waliwaacha wengi vinywa wazi kwa kumbukumbu za mapenzi baada ya kujitokeza hadharani kunengua viuno pamoja na kufarahiana katika sherehe hiyo ya kukata na shoka.

Sherehe hiyo iliyopewa jina I AM ZUCHU iliandaliwa na kampuni ya Wasafi kusherekea hatua aliyopiza Zuchu katika safari yake usanii.

Hafla hiyo iliandaliwa Jumamosi, Julai 18 Mlimani Hall Tanzania wapenzi hao wawili wa zamani hawakuchelea kuipa kilele kwa densi yao maridadi.

Mbosso alipopanda jukwani kupiga kibao chake hodari wa mapenzi, mahodari wa mapenzi, Wema na Diamond waliamka na kuuonyesha ulimwengu maana kamili ya mapenzi.

View this post on Instagram

Look at how Wema Sepetu is looking at Diamond.. 🤩🤩😍

A post shared by Urban News (@urbannews254) on

Wengi waliwashangilia huku densi ya ikishika kasi wakionyesha furaha kwa tabasamu la aina yake.

Haya yanajiri tu miezi mitano baada ya Diamond na Tanasha Donna kuosnyeshana visogo.

Diamond alijitokeza siku chache zilizopita na kueleza kuwa ashapata mpenzi mwengine na kuwa mipango ya kumfungisha pingu za maisha i njiani.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/20/diamond-na-wema-sepetu-watesa-mitandao-wa-densi-ya-mapenzi-wanarudiana/

No comments:

Post a Comment