Wednesday, July 15, 2020

Rais Magufuli ateua Makatibu Tawala wanne akiwemo Mwandishi Mwandamizi wa Gazeti la Nipashe Mashaka Mgeta

Rais John Magufuli amewateuwa  makatibu Tawala akiwemo Mwandishi Mwandamizi wa gazeti la Nipashe Mashaka Bonifance Mgeta kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga.

Rais amemteua Juvenali Jaka Mwambi kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara.

Mwambi anachukua nafasi ya Benaya Liuka Kapinga.

Rais Magufuli amemteua Johari Athumani kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro.

Johari Athumani alikuwa Ofisa katika Ofisi ya Rais anachukua nafasi ya  Aboubakar Asenga.

Rais Magufuli amemteua Ayoub Perro kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.

kabla ya uteuzi huo Perro alikuwa Ofisa katika ofisi ya Upelelezi ya polisi mkoa wa Kigoma na anachukua nafasi ya Twaha Mpembenwe.

Wateule wote wanatakiwa kuwepo Ikulu Chamwino mkoani Dodoma Julai 16, 2020 majira ya saa 4:00 asubuhi.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/15/rais-magufuli-ateua-makatibu-tawala-wanne-akiwemo-mwandishi-mwandamizi-wa-gazeti-la-nipashe-mashaka-mgeta/

No comments:

Post a Comment