Wednesday, July 15, 2020

Jide Uso Kwa Uso Na Zuchu

Mwanamuziki nguli Judith Wambura (lady jaydee) ametimiza ndoto ya mwanamuziki mwenzie Zuchu baada ya kukubari kukutana ye leo julai 15, 2020 jijini Dar es salaam baada ya msanii huyo kuomba kukutana naye ili aweze kujifunza mengi kutoka kwake.

Jaydee ambaye ameweka wazi juu ya kukutana na msanii huyo chipukizi kutoka label ya wasafi inayomilikuwa na mwanamuziki Diamond Platnumz.

“Mrembo wangu Zuchu leo alipita kunisabahi,, Asante kwa kuniheshimu na kunipenda,,Umechagua mikono salama” ameandika Jaydee kwenye ujumbe alituma kwenye ukurasa wake wa Instagram huku akiweka picha yake akiwa na Zuchu.

ikumbukwe hapo jana Zuchu akiwa kwenye mkutano wa kuzinduantamsha lake aliweka wzi kuwa anataka kukutana na lady Jaydee ikiwa ni siku kdhaa bad aya kutimiza ndoto zake za kukutana na Rais John Magufuli.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/15/jide-uso-kwa-uso-na-zuchu/

No comments:

Post a Comment