Rais John Magufuli leo amemteua Dk. Maduhu Isaac Kazi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).
Kabla ya uteuzi huo, Dk. Kazi alikuwa Meneja wa Idara ya Sera za kibajeti na madeni wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano Rais Ikulu, Gerson Msigwa imeekeza kuwa Dk. Kazi anachukua nafasi ya Godfrey Idelphonce Mwambe.
Uteuzi wa Dk. Kazi unaanza leo Julai 12, 2020.
source http://www.bongoleo.com/2020/07/12/rais-magufuli-amtumbua-mkurugenzi-mtendaji-wa-kituo-cha-tic/
No comments:
Post a Comment