Leo Julai 12, 2020 ni siku ya kukumbukwa kwenye macho ya wapenda soka nchini na nje ya nchi kutokana na mchezo wa nusu fainali ya pili ya kombe la shirikisho la Azam, mchezo huu unakuwa wa aina yake kwakua unawakutanisha maasim wawili.
Ni Simba Vs Yanga timu zilizokutana takribani mara 99 mpaka kufikia mwaka 2019 huku rekodi zikiibeba Yanga kutokana na kufanikiwa kushinda takribani michezo 36 huku Simba wakiwa wameshinda mara 28 na wakiwa wametoka sare mara 35.
Uzuri wa mechi hii ni kutokana na uwezo wa wachezaji wake wanaocheza kwenye vikosi vyote viwilii ambao wamesaidia timu zao kuchukua makombe mbalimbali, Simba wamechukua jumla ya mataji 20 huku Yanga wakiwa wamechukua takriabani mataji 27.
Simba na Yanga kukutana leo kwenye hatua ya nusu fainali ni hostori ya aina yake kwakua ni mara ya kwanza kukutana kwenye hatua hiyo tangu kuanzisha kwa kombe hilo la shirikisho ambalo Yanga ameshinda mara moja na Simba mara moja.
Nani anatoka Leo endelea kufuatilia OperaNews kwa Habari za Moja kwa moja kutoka uwanjani.
source http://www.bongoleo.com/2020/07/12/ni-simba-vs-yanga-leo-vita-ya-historia-asfc/
No comments:
Post a Comment