Friday, July 17, 2020

Rais Magufuli amezuia kufanyika sherehe za mashujaa Julai 25, 2020

Rais John Magufuli ameahirisha sherehe za mashujaa zilizopaswa kufanyika Julai 25, 2020 jijini Dodoma.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa.

Rais Magufuli amewataka Watanzania wote kutumia siku hiyo kuwakumbuka na kuwaombea mashujaa wote waliojitoa kwa ajili ya nchi na hata wale ambao wametoa mchango mkubwa katika ngazi mbalimbali ikiwemo mtu mmoja mmoja na familia.

Rais Magufuli amewatakia heri Watanzania wote kuelekea siku hiyo na amewataka kuendelea kudumisha amani, upendo, utulivu na mshikamano.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/18/rais-magufuli-amezuia-kufanyika-sherehe-za-mashujaa-julai-25-2020/

No comments:

Post a Comment