Friday, July 17, 2020

Dondoo za leo: Membe ajitosa rasmi urais, DC anayewania ubunge atumbuliwa, ashukuru na Bibi atuhumiwa kumchoma moto mjukuu wake

Habari ya asubuhi mdau wa Opera News ni siku nyingine ya Jumamosi Julai 18, 2020, matumaini yetu upo salama na karibu katika ujenzi wa taifa.

Tunakukaribusha katika dawati letu la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazopamba asubuhi ya leo.

Habari hizo ni aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe ambaye amejiunga na Chama cha ACT-Wazalendo amechukua fomu ya kugombea urais, DC aliyechukua fomu ya kugombea ubunge atumbuliwa, amshukuru Rais Magufuli na Bibi atuhumiwa kumchoma moto mjukuu wake.

Katibu msomaji wetu;

MEMBE AJITOSA RASMI URAIS

LIYEKUWA Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amechukua rasmi fomu ya kuomba kuteuliwa na Chama cha ACT-Wazalendo kuwania urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Membe (66), alikabidhiwa fomu hiyo jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu, ikiwa ni siku moja tangu ajiunge rasmi na kupokewa na chama hicho.

Wakati wa kuchukua fomu jana, Membe aliyebobea katika masuala ya diplomasia, aliambatana na mkewe, akiwa mwanachama wa kwanza wa ACT-Wazalendo kuchukua fomu ya kuomba kuwania urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Soma zaidi

DC ANAYEWANIA UBUNGE ATUMBULIWA, ASHUKURU

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi, ameeleza sababu ya kuchukua fomu kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuteuliwa kuwania ubunge wa Shinyanga Mjini.

Katambi amesema iwapo atafanikiwa kuteuliwa na chama na kushinda ubunge katika jimbo hilo, ataisaidia Shinyanga kupata maendeleo kama alivyofanya Dodoma.

Jana, Rais Magufuli alimteua Joseph Maganga kuwa Mkuu wa Wilaya Dodoma, kuchukua nafasi ya Katambi. Baada ya Ikulu kutoa taarifa ya uteuzi huo, Katambi alimshukuru Rais Magufuli kwa kumwamini na kumteua kuwa mkuu wa wilaya, akitumikia nafasi hiyo kwa miaka miwili.

Soma zaidi

BIBI MATATANI TUHUMA ZA KUMCHOMA MOTO MJUKUU

JESHI  la Polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia Daria Frank (55), mkazi wa Mamba wilayani Moshi kwa tuhuma za kumuunguza na moto mtoto wa miaka sita kuanzia chini ya kitovu hadi juu ya magoti.

Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Emmanuel Lukula, alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea Julai 10, mwaka huu, majira ya saa 11:00 jioni katika maeneo ya Mamba.

Lukula alisema mtuhumiwa huyo ambaye ni bibi mzaa baba wa mtoto huyo, alimfanyia kitendo hicho cha ukatili mtoto huyo (jina linahifadhiwa) ambaye ni mwanafunzi wa chekechea katika Shule ya St. Paul Albert.

Soma zaidi

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/18/dondoo-za-leo-membe-ajitosa-rasmi-urais-dc-anayewania-ubunge-atumbuliwa-ashukuru-na-bibi-atuhumiwa-kumchoma-moto-mjukuu-wake/

No comments:

Post a Comment