Monday, July 20, 2020

Magufuli Ataja Kigezo Anachotumia Kuteua

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AWAAPISHA MABALOZI WATANO IKULU CHAMWINO ...Rais John Magufuli amesema undugu sio moja ya vikwazo vinavyofanya ashindwe kumteua mtu yoyote kwenye nafasi ya uongozi kwenye serikali ya awamu ya Tano.

Rais Magufuli amesema hayo leo Julai 20,2020 jijini Dodoma wakati wa hafla ya kuwaapisha viongozi aliowateua amesema kitu kikubwa anachikiangalia ni utendaji wa mtueli na si kitu kingine.

“Kuna wateule wawili wote ni watu wa Ireje kule Mbeya na wote nimewateua kwakua kigezo cha undugu, eneo wala udini haziangaliwi kwenye kuteuliwa kinachofanya watu wateuliwe ni utendaji wao na sio undugu wao wala udini hata eneo wanalotoka hawa wanaweza wakawa wanajua nahata wamesoma pamoja lakini ni wachapakazi” amesema Rais Magufuli.

Ikumbukwe mapema Julai 18, 2020 Rais Magufuli alifanya uteuzi wa nafasi kadhaa baada ya baadhi ya waliokuwa wameshikilia nyadhifa hizo kwenda kwenye majukumu mengine.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/20/magufuli-ataja-kigezo-anachotumia-kuteua/

No comments:

Post a Comment