Thursday, July 16, 2020

Membe: Nimekuja Kuleta Furaha Kwa Wananchi

ImageMwananchama mpya wa chama cha ACT Wazalendo, Bernard Membe amesema amejiunga na chama cha ACT ili kuleta furaha kwa wananchi wa Tanzania ambao hawana furaha kutokana na uongozi wa sasa.

Membe amesema hayo alipokuwa anatambulishwa rasmi kwenye chama hicho leo Julai 16,2020 kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mlimani City ikiwa ni hotuba yake ya kwanza kama mwananchama wa chama hicho.

“Nimejiunga na chama hiki ili kufanya kazi na viongozi ambao ni waahanga kama mimi ili kuleta uhuru na maendeleo kwa wananchi ambao wanatakiwa kufaidi na kuwa na furaha maana watanzania wengi hawana furaha kama zamani“ Amesema Membe.

Membe ameongeza kuwa amejiunga chama hicho sababu chama hicho hakijawatenga watu wengine wala kukaa kimya kipindi wanapokutwa na matatizo mbalimbali.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/16/membe-nimekuja-kuleta-furaha-kwa-wananchi/

No comments:

Post a Comment