Saturday, July 11, 2020

Rais Magufuli amepitishwa leo kugombea Urais baada ya kuibuka kwa ushindi wa kura nyingi

Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM)  umempitisha mgombea wake, John Magufuli kugombea nafasi ya urais katika Uchaguzi Mkuu ambao unatarajia kufanyika Oktoba, 2020.

Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa CCM amepitishwa leo baada ya kupata kura za ndio 1822 zilizopigwa jijini Dodoma.

Kwa upande wa Zanzibar jana alipitishwa Dk. Hussein Mwinyi kugombea nafasi ya urais Zanzibar kwa tiketi ya chama cha CCM.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/11/rais-magufuli-amepitishwa-leo-kugombea-urais-baada-ya-kuibuka-kwa-ushindi-wa-kura-nyingi/

No comments:

Post a Comment