Saturday, July 11, 2020

Jeshi la posili limemkamata dereva aliyesababisha vifo 10 mlima Kitonga

Jeshi la Polisi mkoani Iringa limefanikiwa kumkamata dereva aliyesababisha ajali ya basi lililoua watu 10 na wengine zaidi ya 30 kujeruhiliwa katika eneo la Kitonga Wilayani Kilolo mkoani Iringa.

Dereva huyo baada ya kutokea kwa ajali hiyo alikimbia kusikojulikana na jeshi la polisi kuanza kumsaka.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa, Juma Bwera alisema dereva huyo ambaye anaitwa Said Hassan Said wamemkamata mkoani Mbeya akiwa amejificha nyumbani kwa baba yake mdogo.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/11/jeshi-la-posili-limemkamata-dereva-aliyesababisha-vifo-10-mlima-kitonga/

No comments:

Post a Comment