Mgombea urais Zanzibar (CCM), Dk. Hussein Mwinyi amesema akichaguliwa kuwa Rais atamuiga Rais John Magufuli katika kupambana na rushwa, uzembe na ubadhirifu.
“Nikichaguliwa kuwa rais wa Zanzibar nitatumia staili ya Magufuli katika kupambana na rushwa, uzembe na ubadhirifu,” amesema Dk. Mwinyi.
Aliongezea kuwa “Ninawaahidi wananchi wa Zanzibar nitasimamia hayo. Wanaosema mimi mi mpole wasubiri wanione”
Dk Mwinyi jana alipitishwa kuwa mgombea Urais Zanzibar baada ya kushinda kwa kupigiwa kura 129.
source http://www.bongoleo.com/2020/07/11/dk-hussein-mwinyi-wanaosema-mimi-ni-mpole-wasubiri-wanione/
No comments:
Post a Comment