Friday, July 17, 2020

Rais Magufuli amemtumbua Ole Sendeka, Katambi na makatibu wakuu wa wizara

Rais John Magufuli amefanya uteuzi  kwa viongozi mbalimbali huku akimteua Dk. Jumanne Fhika kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe.

Kabla ya uteuzi huo, Dk. Fhika alikuwa ofisi ya Rais na anachukua nafasi ya Christopher Ole Sendeka.

Rais amemteua DK. Aloyce Nzuki kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii.

Kabla ya uteuzi huo Dk Nzuki alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii anakwenda kuchukua nafasi ya Prof. Adolf Mkenda.

Rais Magufuli amemteua mhandisi Anthony Sanga kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji.

Kabla ya uteuzi huo mhandisi Sanga alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji anaenda kuchukua nafasi ya Profesa Kitila Mkumbo.

Aidha, Rais Magufuli amemteua Dk Allan Kijazi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/17/rais-magufuli-amtumbua-ole-sendeka-katambi-na-makatibu-wakuu-wa-wizara/

No comments:

Post a Comment