Thursday, July 16, 2020

Dondoo za leo:Lissu atema cheche kwa jeshi la polisi kutaka majina ya wagombea, Lema asema CCM imefurika wagombea kama usajili wa darasa la kwanza na Fahamu mambo yanayochochea watu kukimbilia ubunge

Habari ya asubuhi mdau wa Opera News ni siku nyingine ya Ijumaa Julai 17, 2020, matumaini yetu upo salama na karibu katika ujenzi wa taifa.

Tunakukaribusha katika dawati letu la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazopamba asubuhi ya leo.

Habari hizo ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu atema cheche kwa jeshi la polisi kutaka majina ya wagombea wao kulikoni polisi kutaka majina hayo?, Lema asema wagombea CCM wamefurika kama wanaandikishwa darasa la kwanza na mwisho Fahamu sababu zinazochochea watu wengine kukimbilia ubunge.

Karibu msomaji wetu;

LISSU ATEMA CHECHE KWA JESHI LA POLISI KUWATAKA KUPELEKA MAJINA YA WAGOMBEA WAO

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maebdekeo (Chadema), Tundu Lissu amesema jeshi la polisi halina mamlaka na mchakato wa uteuzi wa wagombea.

Lissu ambaye alikuwa mbunge wa Singida Mashariki amesema Mkuu wa Polisi Wilaya ya Nzega Mayala amevuka mipaka ya mamlaka yake.

“Jeshi la polisi halina mamlaka wala jukumu lolote kuhusiana na mchakato wa uteuzi wa wagombea uchaguzi ndani ya vyama vya siasa au kwenye Tume ya Uchaguzi,” aliandika Lissu katika ukurasa wake wa Twitter.

Soma zaidi

LEMA ASEMA CCM WAMEFURIKA KUGOMBEA KAMA USAJILI WA DARASA LA KWANZA

Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, amesema wagombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wamefuriki utafikiri kuna uandikishwaji wa darasa la kwanza.

Lema amesema aliyekuwa mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Peter Msigwa, amemjulisha watia nia wa CCM wamefika 96.

Soma zaidi

UCHAGUZI TANZANIA: FAHAMU YANAYOCHOCHEA WATU KUKIMBILIA UBUNGE

 

Kuporomoka hadhi ya utumishi wa umma, kazi za kitaaluma kutothaminiwa, maslahi hafifu, hofu ya kutumbuliwa, usalama mdogo wa kazi, mazingira magumu ya siasa na kuwa njia rahisi ya kupata mafanikio, kutoa michango kupitia siasa, uhaba wa mifumo ya taasisi huru, kutafuta fursa za kuteuliwa ni miongoni mwa sababu zinazotajwa kuchochea wimbi la watumishi wa umma na wafanyakazi wa sekta binafsi kukimbilia ubunge mbali ya ile ya kutanuka demokrasia kuelekea uchaguzi mkuu wa urais, ubunge na madiwani mwezi Oktoba mwaka huu 2020.

Idadi kubwa ya watumishi wa umma na wafanyakazi sekta binafsi wametia nia ya ubunge kupitia chama tawala CCM kuliko vyama vya upinzani ambavyo vimekuwa na idadi ndogo hali ambayo imeibua mjadala juu ya taswira ya chama tawala na vile vya upinzani mbele ya wapiga kura.

Dalili za kuibuka wimbi la watia nia lilianza kuonekana wakati wa uchaguzi mkuu uliopita wa mwaka 2015, ambapo makada 42 walijitokeza kuomba ridhaa ya kuteuliwa CCM ili kuwania nafasi za urais, ikiwa ni idadi kubwa inayotajwa kufungua njia ya joto kali miongoni mwa watu kushiriki siasa kutoka utumishi wa umma na sekta binafsi.

Soma zaidi

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/17/dondoo-za-leolissu-atema-cheche-kwa-jeshi-la-polisi-kutaka-majina-ya-wagombea-lema-asema-ccm-imefurika-wagombea-kama-usajili-wa-darasa-la-kwanza-na-fahamu-mambo-yanayochochea-watu-kukimbilia-ubunge/

No comments:

Post a Comment